![]() |
| Jermaine Grant |
Raia wa Uingereza ambaye ni mwislamu mwenye msimamo mkali, amefikishwa katika mahakama moja katika mji wa Mombasa nchini Kenya kujibu mashtaka ya ughaidi yanayomkabili.
Mashtaka yanasema kua Jermaine Grant, mwenye umri wa miaka 29, alishirikiana na Samantha Lewthwaite, mjane wa mlipuaji mwingine wa London Jermaine Lindsay anayetafutwa vibaya sana mpk dk hii.
Grant -alikamatwa mwezi Disemba mwaka jana - tayari anakabiliwa na kosa lingine la kuingia nchini Kenya kinyume cha sheria, na pia anahusishwa na ulipuaji mabom nchini Kenya na London. Mwanasheria wa serikali ya Kenya Jacob Ondari anadai kua Grant na Bi. Lewthwaite walishirikiana kutekeleza njama zao nyingi za ughaidi na uhalifu ktk nchi mbalimbali duniani.
Bi. Lewthwaite,(28) ambaye ni mjane wa mtuhumiwa mwingine wa malipuzi ya mabom nchini London, anasakwa na serikali ya Kenya na inaaminika anasafiria paspoti bandia. Mume wake alijilipua mwenyewe katika kituo cha treni ya chini ya ardhi mjini London tareh 7 mwezi julai mwaka 2005 ambapo aliuwa watu 26.
Upande wa mashtaka unadai kua mtuhumiwa pamoja na raia watatu wa Kenya, wakipanga njama ya kutumia milipuko walikusudia kuwaua raia wengi.
Kesi hii ilishindwa kuanza mapema jumatano kwa sababu hati za Grant kuhusu uhalifu wake hazikukamilika, na hivyo kuhairishwa mpk hapo document zote zitakapokamilika.
Source: Idhaa ya BBC Kiswahili

0 comments:
Post a Comment