Home »
» MWANAMKE HUYU ANASAKWA KWA KUTOROSHA MTOTO NA PESA SH MIL 15 HUKO MAKAMBAKO
MWANAMKE HUYU ANASAKWA KWA KUTOROSHA MTOTO NA PESA SH MIL 15 HUKO MAKAMBAKO
Mwanamke Queen Daniel Chonya (26) anayedaiwa kumtorosha mtoto na kukimbia na kiasi cha shilingi milioni 15 za mumewe
Mwanamke mkazi wa mji wa Makambako wilaya ya Njombe mkoa wa Njombe Queen Daniel Chonya (pichana juu) anatafutwa na mume wake mfanyabiashara wa mji wa Makambako Timoth Mbuma kwa tuhuma za kumtorosha mtoto pamoja na kukimbia na kiasi cha fedha kiasi cha shilingi milioni 15.
Akizungumza na http://www.francisgodwin.blogspot.com/mfanyabiashara huyo Bw Mbuma amesema kuwa mwanamke huyo ametoroka na mtoto wa kiume mwenye mwaka mmoja na miezi mitano anayeitwa Given au Juniour na kuwa mwanamke huyo mkazi wa Malangali wilaya ya Mufindi ambaye ameishi naye kwa miaka minne sasa katika eneo la Mwembetogwa mji wa Makambako.
Ameongeza kuwa kabla ya kutoweka yeye na mkewe huyo hapa kuwa na ugomvi wowote na kuwa machi 19 siku ya jumatatu asubuhi ambapo alimuita dukani kwa ajili ya kutumwa bank ya NBC kupeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 15 .Baada ya kupewa fedha hizo alikwenda nyumbani na kufungasha baadhi ya vitu kama nguo na vyombo na kutoweka na kuwa mwanamke huyo anasemekana yupo jijini Mwanza ama jijini D'Salaam na kuwa hadi sasa tukio hilo limeripotiwa polisi kwa kumbukumbu namba MKB/RB/709/12 na kuwa kwa yeyote mwenye taarifa anaweza kutumia namba 0752242464 au 0786505524 ama 0655505524 kuwa kubwa hapa anahitaji mtoto na kuwa mtu yeyote mwenye taarifa sahihi alipo mwanamke huyo atazawadiwa donge nono
Habari kamili bofya: http://www.francisgodwin.blogspot.com/
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:
Post a Comment