Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanachama wa Chama cha kuweka Akiba na Kukopa cha URSINO na REGENT (URESCO) kuwa na utaratibu maalum wa kukusanya madeni ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote watakaochelewa kulipa madeni yao.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliyasema hayo jana wakati akifungua SACCOS hiyo iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti huyo wa WAMA aliendelea kusema kuwa ili SACCOS iweze kuendelea ni lazima ijiwekee utaratibu wa kutoa mafunzo na semina mbalimbali za kuwajengea uwezo wanachama wake katika uendeshaji na kusimamia miradi ya jamii.
Kwa habari kamili bofya: http://daresalaam-yetu.blogspot.com/

0 comments:
Post a Comment