WANAFUNZI wa kike zaidi ya 14 katika shule ya msingi Ilala katika Manispaa ya Iringa wamekubwa na ugonjwa wa ajabu wa kuanguka na kuweweseka (kusema maneno yasiyojulikana) kwa zaidi ya wiki moja sasa .
Mwalimu mkuu wa shule hiyo John Nyoni aliueleza mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com leo shuleni hapo kuwa tatizo hilo la wanafunzi kuanguka na kuweweseka lilianza kuwakumba wanafunzi hao zaidi ya wiki mmoja sasa.
Nyoni alisema kuwa awali alianza kuanguka mwanafunzi mmoja ila kila wakati kwa kipindi cha wiki mbili sasa wanafunzi wamekuwa wakianguka na kufikisha idadi ya wanafunzi 14 hadi leo.
Alisema kuwa wanafunzi ambao wamekuwa wakikumbwa na tatizo hilo ni wale wa kike ambao ni darasa la saba na kuwa mara baada ya kuanguka pindi wanapoamka wamekuwa wakikimbia na kusema maneno ambayo ni vigumu kwa mtu mwingine kujua maana na maneno hayo.
Aliwataja wanafunzi ambao wameanguka kuanzia juzi hadi leo kuwa ni Afsa Mkelemi, HUsna Lwila, Subira Hamisi, Regina Mlowe, Anna Hongoli, Ramla Yassin , na Neema Raphael na kuwa wanafunzi hao ndio walioanguka kuonekana kuzidiwa zaidi .
Hata hivyo mkuu huyo wa shule alisema kuwa tayari uongozi wa shule hiyo umechukua hatua mbali mbali za kutatua tatizo hilo ikiwemo ya kuwaita viongozi mbali mbali wa madhehebu ya dini zote .
Pia alisema asubuhi ya leo uongozi wa shule hiyo ulimwita askofu Dkt Boaz Sollo wa Kanisa la Overcomrs ambaye amefanya maombi katika shule hiyo na hali kutulia na wanafunzi kuendelea na masomo yao kama kawaida.
Aidha alisema kuwa uongozi wa shule hiyo kupitia viongozi wa serikali ya mtaa na kata umeomba kuitishwa mkutano wa hadhara siku ya jumamosi kwa ajili ya kulizungumzia tatizo hilo .
Home »
» MADENT WA SHULE YA MSINGI ILALA WAKUMBWA NA UGONJWA WA AJABU, WAKUWEWESEKA
MADENT WA SHULE YA MSINGI ILALA WAKUMBWA NA UGONJWA WA AJABU, WAKUWEWESEKA
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment