Home » » END OF THE ROAD

END OF THE ROAD

Tina naomba uweke hii kwa sweethome,  nahitaji msaada ila kama sitapata ushauri wa maana  mnaweza kusikia msiba wa msaani mwingine very soon


Mimi ni msanii ya bongo movie(jina kapuni) kama unijuavyo ingawa nimekua kimya sana siku hizi kutokana na matatizo ya kifamilia yaliyonikumba hivi karibuni.


Mwishoni mwa mwaka 2010 wakati nipo very busy na ninafanya vizuri tu kwenye swala zima la filamu, niliamua kumchukua mdogo wangu toka kijijini aje dar kusihi nami maana maisha yangu yamekua mazuri na nilitaka kuwapunguzia wazazi mzigo wa malezi. Basi dogo kaja tukaishi kwa vizuri  bila tatizo, ila baada ya kama miezi kadhaa nikamuona ameanza kuchangamka sana tofauti na alivyokuja, ila on the other hand nikajua aah jiji tu limemkubali . loooh..... kumbe usilolijua ni kama usiku wa kiza, mdogo wangu amekua nauhusiano wa kipamapenzi na mchumba wangu right under my nose, na sikujua kabisa na isitoshe she is only 17. 


Sasa juzi kati mchumba (jina kapuni maana pia nyinyi mnamjua ni mwana bongo muvi pia) namuona ameanza kunidharau na kila nikipika hali na kuna vimanenoneno amekua akivisema kila mara ambavyo vikawa vinanifanya nikose raha, eti tukigombana kidogo tu anasema, '' mmh hatujaoana unaanza visa hivi sasa tukioana kweli hapo nitaacha kulala nje?''.  Halafu nikimuuliza amesemaje? anasema harudii mara mbili mbili, wakati alikua hanijibu kabisa hivyo.


Ikabidi nichunguze nijue ni nini kilichomfanya abadilike hivi wakati alikua ananiheshimu tunaheshimiana sana, hawezi kufanya kitu bila kushauriana, tumekua pamoja kwa muda mrefu sasa ingawa watu wengi hawajui ila hii ishu inaweza kuzua makubwa na nimeona niombe msaada, sasa . Juzi narudi kutoka meeting ya kuhusu filamu flani mpya inayotegemea kutoka mwisho wa mwezi huu namkuta mjamaa na mdogo wangu kwa bed  yangu,  sikuamini macho yangu, nikasimama hapo km dk 5 nzima na wao hawakusoge wala kujigusa mdogo wangu anaonekana kuogopa ila jamaa anaonekana hana wasiwasi hata tone moja, wakati nimesimama pale nawaza nikachukue kisu niwachomechome wote na mm niunge segerea au nifanye nini? nikaamua kutoka nje wala mjamaa hakunifata basi, nikaamua kutoka kwenda kwenye kipab kimoja mitaa ya Sinza nikakaa nakunywa sana, na mpaka kesho yake najikuta nyumbani sijui nimefikaje na sina simu zangu hata moja, mdogo wangu hayupo sijui kaenda wapi na inasemekana ana mimba kutokana barua alioniachia nilioikuta huko chumbani kwake.


Tatizo ni sisi tulishaambiwa na tunajua kwamba tumeadhirika na hata tulipokua tunataka kuoana tulikua tusizae , sasa kwanini jamaa kanifanyia hivyo kwa mdogo wangu? kwanini kalala na kumtia mimba mdogo wangu ilhali anajua hali yetu kiafya? mtu km huyu ninamfanyeje? au nijimalize tu mwenyewe ili nisiishi kuona mdogo wangu anateseka? yaani hapa hata sina nguvu hata moja ya kuendelea na filamu tena, mdogo wangu sijui alipo na wala sitaki kumtafuta maana sijui nitamfanya nini? na huyo jamaa nani atamuhukumu jamani naombeni ushauri wenu, sikuweza kutuma barua hii ktk blog mbalimbali za hapa Dar maana wanatujua wataanza kusambaza maneno kabla sijapata suluhu... naombeni ushauri kabla hamjazika msanii mwingine au wengine soon...


Please sweethome adimn ficha  jina na email yangu
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

14 comments:

Anonymous said...

Duuh, ngoja nifikirie cha kukuambia dada hapa sio pa kutoa ushauri wa pupa, ila pole sana sana jamani

Anonymous said...

pole sana jaman mh huu kweli ni mtihani ila mi sikushauri ujiue hilo ondoa kabisaa mie naona kaa kwanza utulize akili halafu ndo utajua chakufanya ila uschukue maamuzi ya haraka japo inauma sana sana

Anonymous said...

cha kumshauri ni athamini maisha yake na sio maisha ya mtu mwingine sio mchumba wala mdogo wake, akaze moyo awasamehe moyoni na aendelee na maisha yake, huyo mchumba moyo wake utamsuta maisha yake yote kwani alijua ameathirika lakini bado akadiriki kulala na mdogo wake

Anonymous said...

asiue wala asigombane nao tena ikiwezekana aongee na ndugu zake kama mama au baba ili wafahamu hali halisi kuliko akikaa nacho kimya moyoni ndio kitazidi kumsumbua, na mdogo wake amekimbia kwasababu anajua alichofanya sio sahihi na anastahili adhabu, lakini ni M'Mungu peke yake ndio atakayejua adhabu ya kumpa

Anonymous said...

pole sana dada, malipo ni hapa hapa duniani, mdogo wako alijua wee una maisha ya raha bila kujua kuwa wee na mchumba mmeathirika na ukute mpaka sasa hv hajajua bado, atakapojua atajuta na ndio itakuwa adhabu yake hayo majuto ni adhabu itakayomhaunt yeye for the rest of her life.....dada huna haja ya kujiua hata kidogo tena mshukuru Mungu kwani umeona makucha ya mchumba kabla hujaingia nodani, na chonde chonde hata akuombe msamaha vipi huyo mchumba usimkubali tena, wako wanaume wengi watakaokupenda wewe kwa hiyo hali yako...una thamani kubwa kuliko machozi yanayokudondoka, usisahau kumuomba Mungu kwani ni yeye pekee ndio atakayekupa nguvu za kuendelea na maisha yako............liv

Anonymous said...

Yaani dear kwanza sijajua kama huyu dada familia yake inajua kama yeye na mumewe/mchumba ni positive ..kama familia inajua basi sina budi kuieleza familia yangu story yote pia nitamchukulia hatua huyo kaka maana anasambaza ugonjwa kwa makusudi coz anajitambua hivyo kunasheria nazani zakumshukulia mtu anayesambaza kwa makusudi.Na mdogo wangu nitamwambia yote toka nimemtoa kijijini hadi alivyofika dar ni kwaupendo wangu so yeye hakunipenda na hakudhamini mchango wangu so nitamwambia wazi sisi ni waathilika so aende akapime nae na hayo ni malipo ya usaliti wake kwangu.nahuyo jamaa achane nae coz kuugua ukimwi sio kufa ila jamaa ndio atamwahisha kufa bora abaki mwenyewe afate ushauri..ni hayo yangu tina

Admin said...

nilivyoelewa kutokana na alivyoandika, sidhani km familia inajua, nafikiri wameliweka jambo hili siri, sasa hapo itakua mbaya zaidi maana ndio siri itabidi ifichuke sasa....

Anonymous said...

Maisha yako ni jambo la msingi sana kuliko hao unaowathamini wakati wao hawakukuthamini,stress lazima ziwepo ila nenda kwa washauri jikubali jipe matumaini songa mbele na masiha yako kwann udhulumu nafsi yako? Kwa sababu ya watu flan ? Ure beutiful fanya kazi mama jali maisha yako ,waambie wazazi maana hujui dogo yuko wapi waarifu basi we kaza buti enjoy wazo la kujiuwa tupa kule kula maisha mama

Anonymous said...

jamani pole sana dada wa watu,,, Najua upo ktk wakati mgumu sana. Ushauri wangu achana na huyo jamaa, nimesikitika kuona kwamba anausambaza ugonjwa bila ya aibu na woga tena kwa ndg yako kabisa, hakika huyu ni muuaji,,, khs mdogo wako inaonekana una mapenzi nae,,, plz achana na mawazo ya kujitoa maisha,,,Endelea na maisha yako,,, rudi kwenye kazi zako, jichanganye na watu km kawaida, ila tafuta mtu uweze kumuelezea kuliko kukaa nacho kimya,,,, pole sana Mumgu akupe nguvu,

mental health promoter said...

Pole mwaya ila muombe tu mungu akupe nguvu na muongozo usijisikie quility sana kwa mdogo wako ingawa ni mdogo kiumri ila inaonyesha alikua anajua anachokifanya angekua innocent angekuambia hata kama alibakwa na huyo mjamaa ni wa kumuanika hadharani kwa kumuharibia mtoto mdogo maisha yake ili dunia imuadhibu kabla hajaenda mbele ya haki na wewe jaribu kuongea na watu wako wa karibu unaowaamini ili wakusupport katika huu muda mgumu kwani pombe si kipotezea mawazo kizuri kwa sababu kinacopmromise judgement na reasoning na zaidi ya yote unakua depressed zaidi ikibidi tafuta professional counsellor akusaidie kuaccept hii situation na kumove on kwa support utaweza si minimise tatizo kwani ni kubwa ila hutaki kulifanya kubwa zaidi hapo kuna hatari ya suicide na homicide pole na mungu akusaidie

Anonymous said...

Mhhh..nimakubwa sana hayo , huyo kaka ni mnyama hasa , unyama wakwe ni huko kuthirika kwake alafu ameamuwa kumuambukiza na shemejie. Ushauri wangu ni hivi : Huyo dada asijiuwe haitasaidia kitu , ampeleke huyo kaka police kwa sababu amemtia mtu mimba aliyechini ya miaka 18 , na pili amemuambukiza hiv kwa makusudi , so hayo ni makosa 2 , alafu amtafute mdogo wake amueleze ukweli wote kuhusu yeye na mchumba wake kuwa ni waathirika , na pia akampime mdogo wake ili aweze kuzaa mtoto asiye na maambukizi , ukiwa na hiv hukatazwi kuzaa na unaweza kuzaa na mtoto asipate maambukizo , cha muhimu nikupima ili ijulikane kma fcd 4 zako zimeshuka au la.

Anonymous said...

Kama unaweza tafuta kitu kitakachokusaidia kurefresh mind ikiwezekana hata kwenda may be mikoani, pili usijidhuru kwa namna yoyote ile utampa faida adui yako ya kufaidi matunda mliyochuma wote, tatu achana naye mchumba wako kaanze maisha mapya kivyako, mdogo wako usihangaike kumtafuta coz alipo wanajua yeye na mchumba wako ila atakapokuja kutokea mpe ukweli akapime.

Anonymous said...

pole sana dada,Mungu akupe nguvu ya kukabiliana na haya matatizo.Usijidhuru wala usiwadhuru.huyu mwanaume mungu atamlipia tu alafu mdog0 wako msamehe na um guide throug haya matatizo,apime ajue status yake kama ameathirika aanze kutumia dawa na kumprotect mtoto wake.Mungu awasaidie wote!

Anonymous said...

roho imeniuma kama ni mdogo wangu jamani.Kwanza kabisa huyo dada atulize hasira asije ua kweli maana haya mapenzi kama mjuavyo.Kuna maisha mazuri tu mbele yake hata kama ameadhirika asife moyo jamani apunguze hasira aendelee na usanii wake ila asiishi na mdogo wake for now maana atammaliza.Na amfungulie huyo jamaa mashitaka maana kwanza katembea na kumwambukiza mtoto under 18 years.huyo mwanaume ndio aende segerea kwa kuua.shenz type

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger