Mjamzito wa miezi 8 mkazi wa kitongoji cha Buchegera kijiji cha Tamukeri kata ya Sedeco wilayani Serengeti amelazwa katika hospitali teule ya Nyerere ddh kwa uangalizi mkali wa waganga kufuatia kupigwa na mme wake na kumjeruhi vibaya kisha kumfungia ndani kwa siku 14 bila matibabu kwa kile kinachodaiwa kumpa uji na viazi.
Mjamzito huyo alilazwa wodi ya wazazi si kwamba anatarajia kujifungua bali kutokana na majeraha makubwa ambayo yanamfanya ashindwe kutembea na ujauzito alionao,hali ambayo inawapa kazi za ziada waganga kuhakikisha
wananusuru maisha yake na mtoto.
Inasemekana mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa vinara kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike nchini Tanzania.
Akiongea na Mwananchi Jumapili akiwa wodi la wazazi kitanda no. 26 alikolazwa huku akibubujikwa na machozi kutokana na maumivu yanayomsumbua alianza kwa kusema kuwa anajutia ndoa yake ambayo
amedumu kwa mwaka mmoja.
“Hili ni tukio la pili kubwa kwangu katika umri wangu mdogo wa kuzaliwa na katika ndoa kwa kuwa nilipigwa desemba 2011 kwa kutumia mjeredi wa kupigia ng’ombe tukiwa shambani kisha niliumia na kwenda yumbani kwetu hadi januari 1,2012 nikarudi kwangu tena”alisema kwa kugugumia.
Habari zaidi ingia: Mwananchi...
Habari zaidi ingia: Mwananchi...
Uuwwiii jamani unampigaje mwanamke wewe ukiwa km mwanaume na akili zako? kama sio uonevu huo ni nini? na isitoshe mwanamke mjamzito wa karibia kujifungua mweeh mbona mijitu mingine ina roho mbaya kiasi hiki? halafu kisa eti kakupikia uji na viazi kama ndio hela uliompa ye afanye nini? km unataka kula kuku si ukamnunue .....mmmmmxxxxxhhhhhh(msonyooo) umeniudhi utasema nakujua vile, lione kwanza km we mwanaume kweli kapigane na ukuta basi hiloooo

0 comments:
Post a Comment