Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari akimpa mkono wa pole mjane wa marehemu, Msafiri Mbwambo, Eunice Mbwambo, aliyeuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana eneo la Usa-River.
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Usa-River, wilayani Arumeru mkoani Arusha, Msafiri Mbwambo (32) ameuawa kinyama kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.Mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha na Wilaya ya Arumeru jana, walifurika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, kushuhudia mwili wa Mbwambo ambaye pia, alikuwa fundi ujenzi .
Mbwambo aliuawa na watu wasiojulikana baada ya kupigiwa simu kumwita majira ya saa mbili usiku, wakati akitazama taarifa ya habari eneo la Mji Mwema akiwa na watu wengine.Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Arumeru, Dotnan Ndonde, alisema mara baada ya marehemu kuondoka muda mfupi baadaye, mwili wake uliokotwa eneo la Shule ya Mukidoma, Kusini mwa mji wa Usa-River umbali wa takriban kilomita mbili kutoka alipokuwa.
“Tulimkuta akiwa anavuja damu ilionekana muda si mrefu alikuwa amechinjwa na watu wasiojulikana ambao walikuwa wametoweka,”alisema Ndonde
Mwili wa kada huyo ulichinjwa kuanzia kisogoni na taarifa za uchunguzi wa madaktari jana zilithibitisha kuwa kifo hicho kimetokana na kuchinjwa.
Babari zaidi: Mwananchi...Picha na Peter Saramba
OMG this is so scary now...Lord have Mercy
Home »
» KIGOGO WA CHADEMA ACHINJWA ARUSHA
KIGOGO WA CHADEMA ACHINJWA ARUSHA
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:
Post a Comment