Well, nasikia ndege zetu zinatarajiwa kuruka tena kabla ya mwishoni mwa mwezi ujao na zitafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na miji ya Mwanza na Kilimanjaro.
Tarrifa hii imedaiwa kurepotiwa na Kaimu Mkurugenzi wa ATCL, Paul Chizi, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa tovuti ya shirika hilo..... Director huyo aliendelea kudai kwa sasa shirika linawasubiri maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)) ili waende Misri kukagua ndege itakayochukuliwa na shirika hilo kwa ajili ya safari za ndani ya nchi na kwamba hatua huyo itafutiwa na ya kupata ndege zingine mbili.
Director alisema ; “Watu wanaulizia kuhusu lini tutaanza safari zetu, nawahakikishia kuwa tunajipanga vizuri ili tuwahudumie vizuri tena ndani ya muda mfupi ujao,” alisema Chizi.
Mweeh naomba haya unayoongea yawe ya kweli bwana mkurugenz;i maana Tanzania mmekua mkitia AIBU katika swala zima la usafiri wa anga jamani, kwanza bado nawadai, kuna siku mlicancel safari yangu nikiwa pale ORTambo Airport na mkatuweka pale kwa masaa kumi na kisha kutudumbukiza kwenye ndege ya Kenya iliojaa makande...nilinuna sana siku hio...
Mmanawezaje kukatisha watu ticket na kuwaacha wafike hadi airport na wakiwa katika check in point ndio mnawaambia eti ndege imekanseliwa..?? uuwwiii Tz kila kitu fake jamani sijui ndege nazo mlizitoa china..?? Ila mkinunua MAJUMBA YENU MNANUNUA YA UKWEEEEEEEEE......hehehehehe duuh kuna siku nitamng'ata mtu pua nyie subirieni tu.
Kama waziri mmoja ananunua JUMBA la dola laki saba ($700,000) a.k.a bil 1.1 za kibongo, kweli nchi inashindwa kununua ndege za ukweli jamani?? halafu mbali na ndege uuwwwwiii hio INTERNATIONAL AIRPORT sasa hehehehe hata sitaki kufika huko leo ...ila tulieni tu kuna siku nitarudi na swala la Airport.....
Haya ndege ziliharibika eti zipo matengenezoni uuwwiiiii sipandi hizo ng'oo labda nipewe lift ya bure; ila kulipia afu ije kuzimika njiani tuambiwe kushuka kusukuma lol kwi kwi kwiiiiii no way; hata Ethiopia wanatushinda, Ethiopia wana ndege za ukweee na sio kwamba ni matajiri kuliko sisi, na Madagascar pia wana ndege za ukweli ila maskini sisi tumewapita sana sana ...yaani ngoja niishie hapa maana msije kusema naomba udiwani bure kumbe ni hasira binafsi tu na nchi yangu...ooh sorry correction hasira na Serikali yangu..
PROUDLY TANZANIAN lol kama unabisha nyanyua bango kimya kimya ANDAMANAAAAAA
God bless Tanzania, God bless America and no place else...
Home »
» AIR TZ BACK TO BUSINESS
AIR TZ BACK TO BUSINESS
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:
Post a Comment