Kuna style moja imeingia siku hizi jijini Dar es Salaam napenda kwajulisha wasomaji wangu ili wapate kujihadhari na utapeli huu kwa bahati mbaya wakikutana na kisa kama hiki:
Style hii iliowaliza watu wengi jini Dar es Salaam anakua kama hivi............Unapokua katika yale maeneo ya foleni kali mida ya kwenda kazini ama kurudi nyumbani anatokea mtu kwa mbele kama anavuka na kukuonyesha ishara yaani kama fungua vioo, na kisha anakupa ishara zaidi kua uangalie nyuma ya gari yako, kumbuka wakati huo wewe upo kwenye foleni na hivyo unaconcentrate na magari yanasogee ili na wewe usogee....basi na wakati yule mtu wa mbele yako yupo bize kukupa ishara mbalimbali kumbe ile ni kukuvuruga akili hapohapo utasikia kitu kama kishindo kwa nyuma ya gari lako (ni mtu kajigongesha kwenye gari yako nakujiangusha ili wadai umemgonga) na ni mwenzie wa yule mtu wa mbele kule aliekua anakupa ishara za uongo na kweli kumbe wote nimatapeli wakubwa,
Kumbuka kitendo au vitendo hivi vinafanyika haraka sana yaani kufumba nakufumbua....basi yule mtu anapojigongesha tu kwenye gari wenzake watatokeza pasipojulikana na kulizunguka gari na utakapofanya kosa la kufungua vioo vyako au kushuka toka kwenye gari ndio hapo utakapolizwa kwani kwa speed ya ajabu mwenye kuchukua simu yako, pochi ama breafcase yako au chochote cha dhamani kilicho katika gari yako watafanya hivyo fasta sana, kwani watakua wanakuzunguka nakusema'' oohh umeua umeuaa....'' sasa wewe si utakua na hofu na consern na yule jamaa aliejiangusha pale chini na baada ya dk km 3 hivi unakuta wameyeyuka na wewe uko empty na wakati mwingine wanadiriki hata kukupa kipigo ili tu uogope kujitetea.
Jamani hali ya uchumi imekua mbaya na watu wanatunga njia mbalimbali za kutapeli watu nchini, hii ndio imeanza sasa jijini Dar na inatisha sana,kuweni makini na ukikutana mtu km hivyo kamwe usifungue vioo au kushuka kwa gari, ni matapeli wa mujini hao na hio ndio new style yao..
Home »
» TAHADHARI: STYLE MPYA YA UTAPELI YAIBUKA JIJINI
TAHADHARI: STYLE MPYA YA UTAPELI YAIBUKA JIJINI
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
1 comments:
Duu! bongo ni noumaa!
Post a Comment