Hivi punde kumekua na rumaz katika vyombo vingi vya habari na mitandao na sosho netiwoku kuwa ndugu Lowassa yupo taabani na amepelekwa nchi za nje kwa matibabu zaidi. Ila juzi kati Lowassa ameibuka akionekana yupo ngangari na mamsapu wake kukanusha vikali kuwa hayupo taabani kama watu wanavyodai na wala hakukimbiziwa huko kwa ajili ya matibabu bali alienda nchini Ujerumani kwa nomo check up ya macho yake ambapo dokta wake alimwambia anaendelea poa sana na wala hakuna cha kuhofia...
Lowassa ameweka msisitizo na kusema amerudi na sasa yuko fiti kwa mapambano yoyote na akiwa anatarajia kwenda kakita jimbo la Arumeru kuendelea na kampeni za hapa na pale, na atahakikisha anampigia debe mkwe wake, (Mgombea huyu Sioi Sumari ameoa mtoto wa Lowassa) mpaka kieleweke...
Blog hii inamtakia Mh. Lowassa kila la kheri na afya tele.....
0 comments:
Post a Comment