Home »
» UUWII JAMANI TUMSAIDIE MAMA HUYU
UUWII JAMANI TUMSAIDIE MAMA HUYU
MWANAMKE mmoja, Asia Ally Abeid (35 ) (pichani), mkazi wa mtaa wa Msikitini, Buguruni kwa Mnyamani Dar, amefika katika Ofisi za Global Publishers Ltd na kulia kwa uchungu akiwaomba Watanzania wamsaidie fedha za kulipia vipimo na matibabu kutokana na uvimbe uliopo kifuani kwake. Akizungumza kwa tabu, Asia aliyeambatana na mjomba wake alikuwa na haya ya kusema:
“Mwaka 2006, hiki kidonda na uvimbe unaouona kifuani, ulianza kama kipele kidogo shingoni, taratibu ukakua huku ukiwa na maumivu makali. Nikaenda hospitali ya Amana Ilala wakanipima na kuniambia kuwa ni uvimbe tu, wakanifanyia upasuaji ili kuuondoa lakini baada ya muda uvimbe ukaanza tena kurudi upya na kwa kasi zaidi ya mwanzo.“Nilirudi tena hospitali ya Amana mwaka 2009 ambapo walinifanyia upasuaji wa pili, lakini jambo la kusikitisha baada ya muda mfupi tu, uvimbe ulianza kurudi tena nikafanyiwa upasuaji mwaka 2010 katika hospitali ya Misheni ya Maria Thomas iliyopo mjini Arusha, lakini pia haikusaidia kwani baada ya muda uvimbe ulianza kurudi tena.
“Mwaka jana 2012, uvimbe ulikuwa mkubwa kama unavyouona (ana muonyesha mwandishi kidonda), nikarudi Hospitali ya Amana ambapo waliniambia wao wameshindwa hivyo wakaniandikia niende Muhimbili ambako nilipimwa lakini hawakuona tatizo. “Nimeambiwa niende Hospitali ya Aga Khan kwa kipimo kingine na gharama ni kubwa ni shilingi 450,000.
“Kwa kuwa sina fedha hizo na ndugu zangu kutokuwa na uwezo wa kuzipata nawaomba Watanzania wenzangu wanisaidi ili niweze kuokoa maisha yangu yaliyo hatarini,” alisema mgonjwa huyo.
Aliyeguswa na habari awasiliane na mgonjwa kwa namba 0657 612 231.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment