Japokuwa gazeti hilo halikutaja jina la msichana huyo huku picha zikimuonesha akiwa amefunikwa uso na hivyo kutotambulika kirahisi, kiongozi wa kundi la Rockaz, Chief Rocker ambaye yupo nchini China kimasomo amethibitisha kuwa msichana huyo ni Jackie Cliff ambaye pia ni rafiki yake wa karibu.
Chief Rocker ameuambia mtandao wa Bongo 5 kuwa amethibisha kuwa aliyekamatwa ni Jackie Cliff baada ya kuongea na ubalozi wa Tanzania nchini humo.
“Amekamatwa kweli. Nilivyosikia story ni kwamba ametoka Bongo akapita Thailand akaenda Macau, Macau ndio akakamatwa. Mimi nilijua kwa sababu nilipigia simu watu wa ubalozi baada ya kupata taarifa tu mara ya kwanza nikawapigia watu wa ubalozi nikawaambia ‘bana, ndugu yetu amekamatwa sasa nataka kujua process ikoje kama kuna kumuona ama kama kuna chochote. Kuna ubalozi mwingine mdogo uko Hong Kong wao ndio wakanambia mambo yalivyo kwamba alikuwa yupo yeye na watu wengine wawili, Mtanzania na Mnaijeria, yeye ndiye akakamatwa , hawa wengine baada ya kuona wanataka kukamatwa wakakimbia.” Amesema Chief Rocker.
Chief ameeleza kuwa kutokana na sheria za Macau kuwa tofauti na za bara nchini China, Jackie anaweza asihukumiwe kunyongwa kama ilivyo kwa sheria za bara.
“Inategemea, ukikamatwa Mainland China au labda ukakamatwa Macau au kwa Macau na Hong Kong ni kama huko kwetu, ni kama Tanzania na Zanzibar. Kwa hiyo yeye alikokamatwa ni kama yuko Zanzibar, ni ndani ya China lakini inategemea sheria zake sio kali sana.
“Lakini sasa mpaka wajaji kutokana na mzigo ulioubeba. Wengine wanasema miaka mitatu, wengine minne, wengine wanasema wanatoa kama Hong Kong miaka nane, so inategemea akiwasaidia polisi akisema watu aliokuwa akiwapelekea mzigo wako wapi na wakapatikana, I don’t know.” Chief ameuambia mtandao wa Bongo 5.
Chief ameonesha kumuhurumia Jackie kwa maisha atakayokaa jela nchini China kwa kuwa hafahamu Kichina, hivyo itakuwa ngumu sana yeye kuweza kuwasiliana na mahabusu wenzake katika hali ya kawaida (Ku-socialize).