Home » » FUMANIZI LA MWAKA: BABU WA MIAKA 70 ANASWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE; MUMEWE AAMUA KUSUSA

FUMANIZI LA MWAKA: BABU WA MIAKA 70 ANASWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE; MUMEWE AAMUA KUSUSA

                                  
SIKU chache zilizopita, gazeti moja  maarufu  hapa  nchini liliripoti juu ya fumanizi la babu mwenye umri wa miaka 70, Rafael Mitasio aliyenaswa gesti akiwa na mke wa mpangaji wake. Taarifa tulizozinasa zinadai kuwa mzee huyo amesusiwa mwanamke huyo.

Chanzo chetu cha habari kimedai kuwa, mara baada ya habari hiyo kutoka gazetini, mume wa mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina lababa Tausi aliumia sana.

“Ile habari ilipotoka kwa kweli mume wa yule mwanamke aliumia sana, akaamua heri huyo mzee amchukue kabisa kama ameona anaweza kumtunza kuliko yeye. 
            
“Cha kushangaza yule mzee naye eti anadai wala habari hiyo haijamuumiza na anasema atamuoa kabisa mwanamke huyo ili kuwakata vilimilimi wabaya wake,”kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Mzee Rafael alipotafutwa kuzungumzia kama kweli ana mpango wa ‘kumchukua jumla’ mwanamke aliyenaswa naye wakivunja amri ya sita, alizungukazunguka sana lakini mwisho akasema:

‘’Si mmeshaandika kuwa nimefumaniwa, haya kaandikeni tena kuwa nataka kumuoa kabisa ili mfurahi.”
 
Hata hivyo, fumanizi hilo lilizua kizaazaa cha aina yake hadi likafikishwa polisi.

Hii story Nimeitoa huko MPEKUZI blog, nimeona nishee hapa maana nikituko, babu wa 70 bado anadai lol hapana chezeya mambo flani yaleeee, unaambiwa eji iz nasingi bati e namba lol kafurahiaje alivyosusiwa my wife wake hahahaha
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger